Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 31 Octoba, 2017

Neymar akiwa pamoja na wachezaji wenzake, Luis Suarez na Lionel Messi mazoezini kipindi alipokuwa Barcelona
Meneja wa Barcelona, Erneto Valverde anaamini kwamba, ipo siku Neymar atarejea kwenye klabu yake ya zamani. (Express)

Klabu ya Shanghai Shenhua kinamtaka mshambuliajia wa Brighton na Israel Tomer Hemed, 30.

Ian Wright anasema kwamba, David Unsworth hapashwi kupewa kibarua cha ukocha Everton baada ya kushindwa kuthibitisha uwezo wake katika mchezo wake wa kwanza akiwa kama meneja wa muda.

Luka Modric na Marcelo
Nyota wa Real Madrid, Luka Modric na Marcelo walitofautiana kiasi cha kuanza kurushiana maneno kwenye mchezo wao dhidi ya Girona uliomalizika kwa Real Madrid kuchapwa goli 2-1. (Sun)

Chelsea wako tayari kumpa mkataba mpya kiungo wa kati Cesc Fabregas baada ya kummezea mate mchezaji huyo wa umri wa miaka 30 wa Manchester United.

Mshambuljia Tammy Abraham, ambaye yuko Swansea kwa mkopo anasema anataka kuichezea Uingerea soka ya kimataifa badala ya Nigeria. (Times)

Arsenal wana mpango ya kumsaini mchezaji wa safu ya kati wa Napoli Jorginho 25. (Tuttomercato, kupitia Star)

Wing'a wa Leicester Riyad Mahrez, 26, anaindwa na klabu ya Marseille ya nchini Ufaransa. (Mundo Deportivo)

Mchezaji wa safu ya kati wa Roma na Ubelgiji Radja Nainggolan, 29, anasema kuwa hakuwa na fikra za kuhamia Chelsea msimu uliopita.

Gary Neville
Gary Neville amemfananisha Jose Mourinho na mwanamasumbwi Floyd Mayweather, alipomtetea meneja huyo wa Manchester United.

Everton wanamtaka meneja wa Burnley Sean Dye kuwa meneja wao mpya na huenda wakawasiliana naye katika kipindi cha saa 24 zinazokuja.(Sky Sports)

Mfanyabiashara kutoka Dubai Amanda Staveley anaweza kiununua klabu ya Newcastle United. (Newcastle Chronicle)

Mshambualjai wa England Jermain Defoe anahofia kukosa kucheza kombe la dunia kutokana na kutojumuishwa katika mechi za Bournemouth.

Hatma ya Slaven Bilic katika klabu ya West Ham bado haijulikani.(Mirror)

Klabu ya China ya Meixian Techand imewapa wachezaji wake pauni milioni 3 kila mchezaji kwa kuiwezesha klabu yao kupanda ngazi hadi divisheni ya pili. (Mail)

Philippe Coutinho, 25
Paris St-Germain wamemuorodhesha Philippe Coutinho, 25, kuwa nambari moja kati ya wacheza watakaowawinda msimu unaokuja. (TF1)

Manchester City wanaamini kuwa wanaweza kumsaini mchezaji wa safu ya kati wa Real Madrid Isco, licha ya yeye kuwa na mkataka wa muda mrefu na Real. (Don Balon, kupitia Daily Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 31 Octoba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 31 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/31/2017 01:53:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.