Loading...

Aliyekuwa IGP ateuliwa kuwa balozi


Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Oktoba 26, 2017 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali katika serikali wakiwepo Makatibu Wakuu, Wakuu wa mikoa na kumteua Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania mstaafu (IGP) Ernest Mangu kuwa balozi.

Akizungumza kwa niaba ya Rais, Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Balozi John William Herbert Kijazi amesema kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi huo ili kukamilisha safu ya watendaji ambao watalisaidia Baraza lake jipya la Mawaziri ambalo amelifanyia marekebisho siku za karibuni. 


Miongoni mwa watu ambao wameteuliwa kuchukua nafasi hizo ni mabalozi wawili ambao vituo vyao vya kazi vitakuja kutangazwa baadaye akiwepo aliyewakuwa IGP Ernest Mangu pamoja na Azizi Mlima.

Aliyekuwa IGP ateuliwa kuwa balozi Aliyekuwa IGP ateuliwa kuwa balozi Reviewed by Zero Degree on 10/27/2017 11:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.