Loading...

Anthony Joshua Vs Carlos Takam kuisimamisha dunia leo

Anthony Joshua kuzipiga dhidi ya raia wa Cameroon Carlos Takam
Bingwa wa mkanda wa WBA na IBF katka uzani mzito dunia Anthony Joshua anasema kuwa atapigana kama bingwa wakati alipomzidi uzani mpinzani wake Carlos Takam mjini Cardiff siku ya Jumamosi.

Uwanja wa Principality utabeba idadi kubwa ya watu huku mashabiki wapatao 70,000 wakitarajiwa katika kile waandalizi wanasema kuwa pigano linalouza kwa kasi katika historia ya uwanja huo.

Joshua alikuwa na uzani wa 18st 2lbs wakati alipopimwa siku ya Ijumaa ,ukiwa ni uzani mzito zaidi katika pigano huku Takam naye akiwa na uzani wa 16st 11bs.

Raia huyo wa Uingereza anasema kuwa ana hamu zaidi ya kushinda pigano hilo zaidi ya lile alilopigana na Wladmir Klitschko katika uwanja wa Wembley mnamo mwezi Aprili, licha ya kwamba raia huyo wa Cameroon mwenye umri wa miaka 36 alichukua mahala pake Kubrat Pulev aliyepata jeraha siku 12 kabla ya pigano hilo.


''Bado najihisi kuwa mpinzani'', alisema Joshua mwenye umri wa miaka 28. na kuongeza:

''Amini usiamini ninajihisi kuwa mpinzani .Sitembei na majivuno kwa sababu ninashikilia ubingwa"
Anthony Joshua Vs Carlos Takam kuisimamisha dunia leo Anthony Joshua Vs Carlos Takam kuisimamisha dunia leo Reviewed by Zero Degree on 10/28/2017 02:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.