Loading...

Daktari atumbuliwa kwa sababu ya utoro


Daktari mmoja wilayani Kisarawe amefutwa kazi baada ya kukutwa na makosa mbalimbali yaliyoonyesha kutia hofu juu ya utendaji kazi kwenye majukumu yake ya kila siku.

Uamzi huo wa kumfuta kazi Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mtakayo. Emmanuel Shumbusho umefikiwa na Baraza la Madiwani halmashauri ya Kisarawe mkoani Pwani.

Makosa ambayo baraza hilo la Madiwani limemhukumu nayo Bw. Emmanuel Shumbusho ni pamoja na uzembe, utoro kazini ambapo hajaonekana kazini kwa takaribani siku tisa bila taarifa yoyote kwa mwajiri wake.


Akitoa maamuzi ya kikao cha baraza la madiwani ya kumfukuza kazi mganga huyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamis Dikupatile amesema kwamba wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini mapungufu mengi kutoka kwa mtumishi huyo.

Madiwani wote kwa pamoja walikubaliana na uamzi huo kutokana na uzembe wa daktari huyo katika suala zima la utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi na kusababisha kuibuka kwa usumbufu mkubwa kutokana na kutopatiwa matibabu kwa wakati.
Daktari atumbuliwa kwa sababu ya utoro Daktari atumbuliwa kwa sababu ya utoro Reviewed by Zero Degree on 10/28/2017 07:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.