Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 28 Octoba, 2017

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane akiwa na Casemiro
Manchester United wanamtaka mchezaji wa Real Madrid, Casemiro mwenye umri wa miaka 25.

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho ameiambia Real Madrid kwamba hatomsajili mshambuliaji wao, Gareth Bale, 28.(Diario Gol)

Real Madrid wamewaorodhesha wachezaji watatu wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya Cristiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 32, akiwemo mchezaji wa PSG, Goncalo Guedes, 20, kiungo wa kati wa Gremio Lincoln, 18, na nyota wa Palmeiras Alan Souza, 20. (Daily Mirror)

Chelsea inaandaa dau la Euro milioni 80 kumnunua kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez, 22. (Don Balon)

Barcelona iko tayari kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoinne Griezman kwa dau la £89m msimu ujao (Mundo Deportivo)

Coutinho amekataa uhamisho wa Paris St-Germain mnamo mwezi Januari 2018 na amemtaka ajenti wake kumtafutia uhamisho wa Bareclona. (Sport)

Barcelona italazimika kupunguza kiwango cha madeni iwapo wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool Philipe Coutinho, 25.

Liverpool pia inajiandaa kumnunua beki wa kushoto wa Roma Emerson Palmieri , 23 kwa dau la £22m baada ya kupona jeraha la goti. (Daily Mail)
Ally McCoist anasema kuwa yuko tayari kurudi ili kuwa meneja wa Rangers baada ya kuwasaidia kupanda daraja wakati alipokuwa mkufunzi kutoka 2011 hadi 2015 (Talksport)

Kiungo wa kati wa Leicester Papy Mendy ,25, ambaye yuko katika klabu ya Nice kwa mkopo ana muda mrefu kuihudumia klabu hiyo kulingana na kocha Claude Puel. (Leicester Mercury)

Kampuni ya PCP Partners inataka kuinunua klabu ya Newcastle kwa £300m . (Newcastle Chronicle)

Ununuzi wa beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw, 22, kiungo wa kati wa Everton Ross Barkley, 23, na mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, 28, ulijadiliwa katika mkutano huku wawakilishi wa Newcastle wakikutana na PCP Partners kujadili kuwasajili wachezaji hao.(Daily Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 28 Octoba, 2017  Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 28 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/28/2017 08:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.