Loading...

Conte athibitisha kurejea kwa nyota huyu


Meneja wa Chelsea, Antonio Conte anasema kwamba, N'Golo Kante yuko tayari kurejea uwanjani baada ya afya yake kuimarika.

Meneja huyo ametoa taarifa mpya kuhusu hali ya majeraha ya mfaransa huyo anayecheza nafasi ya kiungo, akiwaambia wanahabari kwamba N'Golo Kante ameshapona jeraha alilopata mwanzoni mwa mwezi uliopita.



“Kante anaendelea vizuri. Nilimuona akiwa na hali nzuri ya kimchezo. Kwa sasa tunatakiwa kuwa na subira, tumpe muda wa kukusanya nguvu zaidi tukisubiria wakati muafaka wa kumjumuisha kikosini. Itakuwa ni rahisi sana kumwambia acheze ipasavyo atakapokuwa na hali nzuri zaidi.”

Majeraha ya Kante yalipelekea matokeo mabaya kwa Chelsea kama ambavyo wengi wanaamini, ambapo Chelsea walipoteza mechi yao dhidi ya Crystal Palace siku kadhaa baada ya mfaransa huyo kuumia na pia kutoka sare ya goli 3-3 na AS Roma kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Alipoulizwa kuhusu Danny Drinkwater, Conte alisema: “Tutakuwa na michezo mitatu kabla ya kwenda kwenye mapumziko na ili kujiridhisha kwamba hali yake iko sawa kwa asilimia 100% labda tusubiri hadi baada ya mechi za kimataifa. Lakini kama nitataka kutumia viungo watatu ndani ya uwanja ni jambo la muhimu akapata nafasi kikosini.”
Conte athibitisha kurejea kwa nyota huyu Conte athibitisha kurejea kwa nyota huyu Reviewed by Zero Degree on 10/26/2017 03:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.