Loading...

Diamond atangaza ujio wa Albam yake mpya iitwayo ''A Boy From Tandale''


Mshindi wa tuzo ya mwanamuziki bora wa kiume Afrika Mashariki kwa miaka minne mfululizo katika tuzo za Afrimma, Diamond Platnumz ametangaza ujio wa albamu mpya aliyoipa jina la A Boy From Tandale.


Hii itakuwa albamu ya tatu kwa mwanamuziki huyo, baada ya Kamwambie na Lala Salama.

Taarifa zimeeleza baadhi ya nyimbo zitakazokuwemo kwenye albamu hiyo ni Number One na Number One Rmx, Nasema Nawe, Bum Bum, Nitampata wapi na Nana.

Mwanamuziki huyo anayetamba na wimbo mpya wa Hallelujah, amesema yupo kwenye maandalizi ya mwisho kutengeneza kazi hiyo ambayo ni maalumu kwa mashabiki wanaopenda muziki wake.

Diamond juzi Jumatano aliutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuwataarifu mashabiki kuhusu kazi hiyo mpya akiandika, “Album soon come, #ABoyFromTandale”.

Kwa mujibu wa taarifa ya MCL, meneja wa mwanamuziki huyo, Salaam Sharaf amesema kwamba, huo ni ujio mpya wa mwanamuziki huyo ambao utakuwa na mambo mengi ya kushangaza ndani yake. Alipotakiwa kuelezea albamu hiyo itauzwa wapi na itasambazwa vipi, Salaam alijibu: “Tuna mengi ya kuzungumza kuhusu albamu hii na namna itakavyowafikia mashabiki wetu, watu wavute subira tutaliweka wazi jambo hili hivi karibuni.”
Diamond atangaza ujio wa Albam yake mpya iitwayo ''A Boy From Tandale'' Diamond atangaza ujio wa Albam yake mpya iitwayo ''A Boy From Tandale'' Reviewed by Zero Degree on 10/13/2017 01:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.