Gazeti la Tanzania Daima lafungiwa kwa siku 90
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk Hassan Abbasi |
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk Hassan Abbasi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ameandika, “Serikali imelichukulia hatua za kisheria gazeti la Tanzania Daima kwa mwendelezo wa kuandika habari za uongo… Taarifa kamili inakuja.”
Ingawa mpaka habari hii inawekwa katika mtandao, Dk Abbasi ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali hajabainisha ni hatua gani wamechukua, uongozi wa Tanzania Daima umesema wamefungiwa kwa siku 90.
Kaimu Mhariri wa gazeti hilo, Martin Malera akizungumza na Mwananchi amesema, “Tumepokea barua ya kulifungia gazeti letu saa 9:36 alasiri, barua ambayo imesainiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.”
Tanzania Daima limekuwa gazeti la tano kufungiwa katika kipindi cha miaka miwili likitanguliwa na Mwanahalisi, Raia Mwema, Mseto na Mawio ambayo yapo kifungoni kwa vipindi tofauti.
Gazeti la Tanzania Daima lafungiwa kwa siku 90
Reviewed by Zero Degree
on
10/24/2017 10:23:00 PM
Rating: