Hazard ataja sababu ya jina lake kutokea kwenye orodha ya wanaowania tuzo ya Ballon D'Or
Hazard anaamini yeye hana nafasi ya kutwaa tuzo hiyo na adaia kwamba, ili afanikiwe kutwaa tuzo yenye heshima kubwa kama hiyo, klabu ya Chelsea italazimika kutwaa mataji yote.
Kwa mujibu wa taarifa ya Sky Sports, Hazard alisema: “Sina nafasi ya kushinda. Naona wachezaji wengi wana uwezo mkubwa zaidi yangu, lakini nafurahia kuwa kwenye orodha ya wachezaji 30 walio bora zaidi na ni kwa sababu tu naichezea klabu ya Chelsea. Nacheza na wachezaji wenye ubora mkubwa wanaonisaidia mimi kuonekana kwenye orodha hii.
“Sijui kama kwa baadae ntapata nafasi ya kutwaa tuzo ya Ballon d'Or lakini haliko kwenye malengo yangu ya sasa. Kwa sasa lengo langu ni kuifurahia kazi yangu nikiwa dimbani.
“Kwa takribani muda wa miaka kumi imekuwa ni nafasi ya Lionel Messi au Cristiano Ronaldo, lakini kwa sasa Neymar na wengine kadhaa wanaanza kuingia, hivyo tusubirie labda zama za Messi na Ronaldo zitakapoisha, ndio tunaweza kupata nafasi kubwa ya kulishindania taji hili lakini kwa sasa haliko kichwani mwangu.
“Tuna nafasi kubwa ya kutwa tuzo ya Ballon d'Or kama tutatwaa mataji yote. Kwa mtazamo wangu, Ronaldo anafaa kupewa heshima hiyo kwa sababu ameshinda michezo muhimu akiwa na Timu yake ya Taifa, ametwaa Taji la Ligi ya Mabingwa (UEFA) na la Ligi kuu ya Uhispania (La Liga). Ili nije kuwa mshindi wa tuzo hiyo siku moja, nitatakiwa kutwaa mataji yote!”
Hazard ataja sababu ya jina lake kutokea kwenye orodha ya wanaowania tuzo ya Ballon D'Or
Reviewed by Zero Degree
on
10/16/2017 08:27:00 PM
Rating: