Loading...

Mpya kuhusiana na majeraha ya Alvaro Morata


Alvaro Morata anaelekea kupona majeraha yake katika paja na kurejea uwanjani hivi karibuni.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika, Morata ataanza mazoezi na klabu yake ya Chelsea wiki hii, lakini hataweza kushiriki katika mchezo dhidi ya Crystal Palace wikendi ijayo.


Morata aliumia wakati Chelsea ikipoteza mchezo kwa kuchapwa goli 1-0 dhidi ya Manchester City kabla ya mapumziko ya michezo ya kimataifa.

Licha ya kupata majeraha hayo, alijiunga na timu yake ya taifa ya Hispania kwa mechi za kimataifa ambapo madaktari waliyafanyia uchunguzi majeraha yake na kumtaka akae nje ya uwanja kwa matibabu zaidi.

Chelsea wamekua wakimfanyia majaribio mbalimbali mchezaji huyo na wanadai hajaumia vibaya sana kama walivyodai madaktari wa timu yake ya taifa.

Amekuwa akifanyiwa majiribio kwenye uwanja maalum wa mazoezi wa Chelsea na anakaribia kurejea dimbani.

Safari ya Chelsea ya Jumamosi kuelekea kuivaa Crystal Palace bado itakuwa ni mapema sana kwa mchezaji huyo, lakini anategemewa kurejea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Roma wiki ijayo.
Mpya kuhusiana na majeraha ya Alvaro Morata Mpya kuhusiana na majeraha ya Alvaro Morata Reviewed by Zero Degree on 10/10/2017 10:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.