Loading...

Mtazamo wa Simon Msuva juu ya mechi ya Simba na Yanga


KIUNGO wa zamani wa Yanga anayechezea Difaa Al Jadida ya Morocco, Simon Msuva amesema mechi ya leo ya Simba na Yanga ni ngumu kutokana na ubora wa kila timu hivyo isionekane mechi rahisi.

Kiungo huyo aliyetimka Yanga mwanzoni mwa msimu huu, alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilicholala mabao 2-1 dhidi ya Simba Februari 25, mwaka huu huku yeye akifunga bao moja.

Akizungumza na Champion, Msuva amesema kuwa, anauona mchezo huo kuwa mgumu kutokana na matokeo ya vikosi vyote kwenye michezo iliyopita. “Siwezi kusema kwamba eti Yanga au Simba mmoja atafungwa kwa sababu kwanza michezo ya namna hii huwa migumu sana mmoja kupata matokeo kwa sababu ya ile hali ya kukamiana kwa wachezaji.

“Pia timu zote hivi karibuni zimefanya vizuri na hata mechi zao za mwisho kabla ya kukutana zimeshinda kwa idadi kubwa ya mabao na hata kwenye msimamo wanalingana pointi.

“Hata viwango vyao uwanjani wanalingana kwa kiasi kikubwa, jambo ambalo linazidi kuutia ugumu mchezo huu, niwe mkweli kwamba tusubiri kuona dakika 90 zitaamuaje. “Timu itakayokuwa na mchezo mzuri basi ndiyo itakayopata matokeo mazuri mbele ya mwenzake,” alisema Msuva.
Mtazamo wa Simon Msuva juu ya mechi ya Simba na Yanga Mtazamo wa Simon Msuva juu ya mechi ya Simba na Yanga Reviewed by Zero Degree on 10/28/2017 08:12:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.