Loading...

Mpya kuhusu N'Golo Kante, ....Je, atacheza dhidi ya Roma? Soma hapa taarifa ya Conte!


Antonio Conte ametoa taarifa mpya kuhusiana na hali ya N'Golo Kante kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Chelsea na Roma usiku wa leo.

Meneja huyo wa 'The Blues' amemkosa nyota huyo kwenye kikosi chake kwa takribani mwezi mmoja sasa, na amekumbana na hali ngumu katika kipindi chote cha majeruhi alichopitia Kante. Chelsea wameshuka kwa pointi tisa nyuma ya viongozi wa Ligi, Manchester City.

Kwa bahati nzuri, Kante amerejea kufanya mazoezi na wachezaji wenzake na amesafiri pamoja na kikosi cha Chelsea kilichoelekea Italia kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Roma. Hata hivyo, Conte hajataka kuthibitisha moja kwa moja iwapo nyota huyo atacheza au hatacheza dhidi ya Roma.


“Ninaujua vizuri sana umuhimu wa mchezaji huyu, lakini nataka kuhakikisha yuko tayari kurejea.” alisema kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya Juventus na kuongeza:


“Natumainia kuwa naye kwenye mechi hii, lakini siko tayari kwa hatari yoyote inayoweza kujitokeza. Kama yeye yuko tayari, basi atacheza.”

Kante alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya 
PFA ya mchezaji bora msimu uliopita ambapo Chelsea ilinyakua ubingwa wa Ligi Kuu na alitoa mchango mkubwa sana kwa klabu yake kufanikiwa kupata mafanikio hayo. Pia alishinda taji hilo akiwa na Leicester City kabla ya kuhamia Chelsea.

Huu ni mchezo wa muhimu kwenye  Ligi ya Mabingwa, na Chelsea watamtaka awe katika hali nzuri ili kupata mafanikio na kufanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo.

Kante, Hazard, Morata na wengineo wanatarajiwa kuanza na kikosi cha kwanza kwenye mechi dhidi ya Roma.
Mpya kuhusu N'Golo Kante, ....Je, atacheza dhidi ya Roma? Soma hapa taarifa ya Conte! Mpya kuhusu N'Golo Kante, ....Je, atacheza dhidi ya Roma? Soma hapa taarifa ya Conte! Reviewed by Zero Degree on 10/31/2017 09:09:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.