Loading...

Zitto Kabwe akamatwa na polisi


MBUNGE wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa nyumbani kwake leo asubuhi na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Chang’ombe.

Jeshi la Polisi bado halijaeleza sababu ya kumakamata, lakini Chama cha ACT Wazalendo, kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Yeremiah Kulwa Maganja wamesema kwamba, sababu ya kukamatwa kwa Zitto Kabwe ni kutokana na mkutano wao wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika Kijichi mwishoni mwa juma.

Inadaiwa sababu za kukamatwa kwake hotuba aliyoitoa Kijichi wakati wa kufungua Kampeni za Udiwani.

Aidha, ACT Wazalendo wameeleza kwamba, wanasheria wa Chama wanashughulikia kujua sababu za ukamatwaji huo Zitto ambaye pia ni kiongozi wa chama hicho.
Zitto Kabwe akamatwa na polisi Zitto Kabwe akamatwa na polisi Reviewed by Zero Degree on 10/31/2017 09:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.