Loading...

Orodha ya wachezaji watakaowania tuzo ya Ballon d’Or 2017


Majina ya wachezaji watano wa kwanza waliotajwa mapema hii leo kuwania tuzo ya Ballon d’Or 2017 ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazili na klabu ya Paris Saint-Germain, Neymar, Paulo Dybala na N’Golo Kante.

Beki wa Real Madrid, Marcelo na mchezaji mwenzake Luka Modric pia ni miongoni mwa waliyotajwa.

Neymar amekuwa msaada mkubwa kwa timu yake ya taifa ya Brazili na klabu ya Barcelona kabla ya kuuzwa katika kipindi cha majira ya joto na kuhamia PSG kwa dau lililoweka rekodi ya dunia ya paundi milioni 222.

Nisawa na Dybala ambae amekuwa msaada mkubwa ndani ya timu ya Juventus mwaka huu wa 2017.

Wakati Kante akifanikiwa kuisaidia klabu ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza kufanya vizuri.

Marcelo ametoa pasi tisa zilizochangia magoli ‘assists’ mwaka 2017 na Modric, wakiwa wameisadia Madrid kushinda kombe la Ligi Kuu nchini Hispania ‘La Liga’ huku wakiiwezesha timu hiyo kutwaa kombe la klabu bingwa barani Ulaya.

Bado majina yataendelea kutajwa huku Cristiano Ronaldo ambaye anashikilia taji hilo akisubiriwa kwa hamu na Lionel Messi akiwa ni miongoni mwa wanao subiriwa lakini pia wapo wachezaji kama Antoine Griezmann na Gianluigi Buffon. 

Orodha ya Majina ya wachezaji waliotajwa kuwania tuzo ya Ballon d'Or hadi hivi sasa 2017

  • Philippe Coutinho (Liverpool)
  • Kevin De Bruyne (Man City)
  • David de Gea (Man Utd)
  • Paulo Dybala (Juventus)
  • Edin Dzeko (Roma)
  • Harry Kane (Tottenham)
  • N'Golo Kante (Chelsea)
  • Robert Lewandowski (Bayern Munich)
  • Marcelo (Real Madrid)
  • Dries Mertens (Napoli)
  • Luka Modric (Real Madrid)
  • Neymar (PSG)
  • Jan Oblak (Atletico Madrid)
  • Sergio Ramos (Real Madrid)
  • Luis Suarez (Barcelona)
Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa orodha ya majina mengine zaidi.
Orodha ya wachezaji watakaowania tuzo ya Ballon d’Or 2017 Orodha ya wachezaji watakaowania tuzo ya Ballon d’Or 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/09/2017 07:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.