Loading...

Tamko la Takukuru kuhusiana na ushahidi wa Nassari na Lema

Valentino Mlowola
WANANCHI wanaopeleka taarifa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) wametakiwa kuwa na subira na kutokishinikiza chombo hicho kuchukua hatua haraka na kutoingiza masuala ya kisiasa katika kazi zake.

Hayo yalisemwa leo na mkurugenzi wa taasisi hiyo, Valentino Mlowola, mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na wabunge Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki na Godbless Lema wa Arusha Mjini ambao hivi karibuni wamekuwa wakipeleka walichokiita ushahidi kuthibitisha madai yao kwamba madiwani wa Arusha waliojitoa katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walihongwa fedha na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ili wachukue hatua hiyo.

Aliwataka wabunge hao na wananchi kwa jumla kufikisha ushahidi wa aina yoyote katika taasisi hiyo na kuiacha ifanye kazi zake kwa utaratibu wa kisheria.
Tamko la Takukuru kuhusiana na ushahidi wa Nassari na Lema Tamko la Takukuru kuhusiana na ushahidi wa Nassari na Lema Reviewed by Zero Degree on 10/17/2017 01:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.