Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 13 Octoba, 2017


Lionel Messi anafikiria kwenda kuanza maisha mapya kwa kuhamia Manchester City katika majira ya joto mwakani.

Manchester United wako kwenye mikakati ya kumnasa beki wa kusho wa Spurs, Danny Rose kwa kiasi cha paundi milioni 50.

Nayo klabu ya West Ham wanamatamanio ya kumsajili kinda wa Hartlepool, Connor Simpson akitabiliwa kuja kuwa Andy Carrol mpya. (Chanzo: The Sun)

Manchester City wako tayari kumsajili Alexis Sanchez ifikapo mwezi Januari endapo bei yake itapungua kwa kiasi cha paundi milioni 20.

Beki wa Bournemouth, Simon Francis ana hamu ya kukutana na Harry Kane kwenye mchezo wao dhidi ya Tottenham wikendi hii.

Naye Slaven Bilic anaamini kwamba watu hawajamwelewa vizuri Goli kipa wa Uingereza na klabu ya West Ham, Joe Hart. (Chanzo: Daily Mirror)

Klabu ya Manchester City inatarajiwa kufanya mpango madhubuti wa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez mwezi Januari. 
(Chanzo: Telegraph)

Robbie Fowler anaamini Manchester United wamekuwa na mwanzo mlaini kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. (Chanzo: Daily Mail)

Katika hali ya utani, Tony Pulis amesema kwamba James McClean hatacheza tena kwenye kikosi chake baada ya kufunga goli lililowatoa Wales nje ya Kombe la Dunia 2018. (Chanzo: Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 13 Octoba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 13 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/13/2017 01:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.