Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 27 Octoba, 2017


Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja atakaa chini  na bodi ya klabu hiyo mwisho wa msimu huu kwa ajili ya kufanya tathmini ya ukufunzi wake. (Express)

The Gunners wako katika mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Stuttgart ambaye ni raia wa Uturuki Berkay Ozcan, 19. (BeinSports)

Mkufunzi wa Watford Marco Silva, ambaye anapigiwa upato kuiongoza Everton amesema kuwa haondoki Watford. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Watford Etienne Capoue, 29, anataka kuandikisha mkataba wa muda mrefu na klabu hiyo.(Evening Standard)

Klabu ya Sevilla inajiandaa kuwasilisha ombi la kumnunua mshambualiji wa klabu ya Monaco raia wa Montenegro Stevan Jovetic, ambaye analengwa na klabu ya Brighton. (Talksport)

Manchester United, Arsenal na Bayern Munich zinamchunguza mshambuliaji wa Barcelona Jose Arnaiz, 22.

Liverpool inataka Euro milioni 150 kumuuza mchezaji anayesakwa na Barcelona Philippe Coutinho - ikiwa ni pungufu ya Euro milioni 50 ya dau walilotaka kulipwa msimu ulioipita.(Mundo Deportivo)

Wamiliki wa Liverpool's walikataa makubaliano yenye thamani ya hadi £1.5bn kuiuza klabu hiyo kwa wawekezaji wanaoongozwa na mwekezaji wa Dubai Amanda Staveley. (The National)

Barcelona huenda ikabadilisha jina la uwanja wake na kuwa Nou Camp Grifols kuanzia msimu ujao.

Klabu hiyo inakaribia kutia kandarasi na kampuni moja ya kuuza dawa yenye na thamani ya £304m. (Catalunya, kupitia Daily Mail)

Mshambuliaji wa zamani wa Celtic Chris Sutton anasema kuwa Pedro Caixinha alikuwa meneja mbaya zaidi wa timu ya Rangers katika historia ya klabu hiyo. (Daily Record)

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho ni sharti ashinde mataji baada ya klabu hiyo kuwekeza vikali kulingana na beki wa zamani wa klabu hiyo Rio Ferdinand.

Liverpool itampatia kinda wa Uingereza anayechezea timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 Rhian Brewster, ambaye alifunga hat-trick mbili katika kombe la dunia , kandarasi nzuri wakati atakapofikisha umri wa miaka 18.(Daily Mail)

Chelsea inajiandaa kumrudisha mkufunzi wake wa zamani Carlo Ancelotti ambaye atachukua mahala pake Antonio Conte.

Liverpool na Newcastle zinajiandaa kumsajii kipa wa klabu ya Porto, Iker Casillas. (Sun)

Arsenal itamuuza mshambuliaji wake Alexis Sanchez kwa dau lisilopungua paundi milioni 30 kwa Manchester United ifikapo mwezi Januari. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 27 Octoba, 2017  Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 27 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/27/2017 02:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.