Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 17 Octoba, 2017
Kwa mujibu wa Jeff Reine-Adelaide, Alexis Sanchez ni mfano bora kwa wachezaji wadogo wa Arsenal.
Isco anasema kwamba, Cristiano Ronaldo ndiye atakayekuwa mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or mwaka huu.
Marcos Alonso amepewa nafasi kubwa ya kuchukua namba ya beki wa kushoto wa klabu ya Barcelona, Jordi Alba. (Chanzo: Star)
Arsenal wako tayari kujaribu kutafuta klabu itakayomnunua Mesut Ozil mwezi january.
Liverpol wanatazamia kumsajili kinda wa klabu ya Sheffield United, David Brooks anayecheza nafasi ya kiungo.
Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane anasisitiza kwamba, Mauricio Pochettino amefanikiwa kumwamsha mpinzani mwenye nguvu aliyekuwa amelala usingizi. (Chanzo: Daily Mirror)
Akiwa na majeruhi wengi, Antonio Conte amefanya tathimini ya wachezaji wake baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Crystal Palace wikendi iliyopita na tayari anatazamia kumtafuta mbadala wa Michy Batshuayi itakapofika mwezi January. (Chanzo: Telegraph)
Arsenal wanapewa nafasi kubwa ya kumnasa nyota wa AC Milan, Andrea Silva msimu huu.
Carlo Ancelotti ataitosa AC Milan akiwa na matumaini ya kuwa meneja mpya wa Klabu ya Juventus katika majira ya joto.
Zinedine Zidane ameshindwa kutengeneza mazingira ya kumnasa mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane.
Mtoto wa George Weah, Timothy amefunga 'hat-trick' ya muhimu wakati timu ya vijana ya Marekani chini ya miaka 17 ilipoibuka na ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Paaraguay.
Seedorf amefichua siri ya kwamba, alisaini mkata na klabu ya Real Madrid akiwa gereji.
Juan Mata amekataa ofa ya kulipwa paundi 375,000 kwa wiki baada ya makato ya kodi ili ajiunge na klabu ya Ligi Kuu ya China.
Dave Whelan anatarajia kuiuza Wigan kwa paundi milioni 15 kwa wachina ndani ya wiki chache zijazo. (Chanzo: Sun)
Jose Mourinho anategemewa kusaini mkataba mpya Manchester United, lakini atafanya hivyo ikiwa atajiaminisha kwamba makubaliano yataliangalia suala zima la mafanikio ya klabu chini ya uongozi wake. (Chanzo: The Guardian)
Manchester City na Barcelona zitaingia katika vita ya kuwania saini ya nyota wa Borussia Dortmund, Julian Weigl.
Manchester United wanatarajiwa kujaribu kuelekeza majeshi yao kwa kiungo wa Sweeden, Rines Arifl.
Barcelona inadaiwa kuwa katika mawindo ya saini za wachezeji watatu wa klabu ya Bayer Leverkusen, Jonathan Tah, Julian Brandt na Leon Bailey.
Swansea wanajadili kuhusu ofa ya beki wa kushoto wa Slovenia Matic Paljk, ambaye ni mchezaji huru hadi hivi sasa. (Chanzo: Daily Mail)
Alvaro Morata anategemewa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Chelsea kwenye mechi ya Klabu Bingwa dhidid ya Roma. (Chanzo: Daily Express)
Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham, Daniel Levy anadai kwamba, Harry Kane ni zaidi ya paundi milioni 200 ambazo PSG walilipa kwa Neymar. (Chanzo: Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 17 Octoba, 2017
Reviewed by Zero Degree
on
10/17/2017 12:27:00 PM
Rating: