Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 10 Octoba, 2017


Paris St-Germain wataitikisa klabu ya Chelsea kwa kujaribu kumsajili N'Golo Kante mwezi Januari.

Vigogo hao wa Ligi kuu ya Ufaransa pia walijaribu kumsajili Kante baada ya kuonyesha kiwango kikubwa wakati akitwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na Leicester City, lakini nyota huyo akawa amechagua kujiunga na Chelsea baada ya timu yake ya taifa ya ufaransa kufika Fainali ya michuano ya EURO 2016. (Chanzo: SillySeason)

Manchester United wana matumaini ya kumsajili mlinzi wa Tottenham Danny Rose,27, mwezi Januari (Chanzo: Tuttomercato, kupitia Talksport)

Barcelona wanajitahidi kumpata mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, kwa pauni milioni 89 kabla ya thamani ya mchezaji huyo wa umri wa miaka 26 kupanda msimu ujao (Chanzo: Mundo Deportivo, kupitia Daily Mirror)

Paris St-Germain wako katika mikakati ya kumuuza wing'a Angel di Maria, 29, kwenda China mwezi Januari.(
Chanzo: TMW, kupitia The Sun)

Arsenal wameafikia makubaliano na wing'a wa zamani Marc Overmars,44, ya yeye kuondoka Ajax na kuwa mkurugezi wa kandanda kuanzia msimu ujao.(
Chanzo: Tuttomercato, kupitia Daily Express)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa zamani wa Italia Andrea Pirlo, 38, hajakana mpango wa kujiunga na kikosi cha makocha, kufuatia uamuzi wake wa kustaafu misho wa msimu wa MLS. (
Chanzo: Gazzetta dello Sport, kupitia London Evening Standard)

Meneja wa Manchetser United Jose Mourinho alikuwa ndani ya umati wa watazamaji wakati wa ushindi wa Austria dhidi ya Serbia, kumtazama wing'a wa Eintracht Frankfurt, Mijat Gacinovic, 22.

Mshambuliaji Newcastle Aleksandar Mitrovic, 23, ananyemelewa na Brighton hapo Januari. (Chanzo: Daily Mirror)

Everton wanammezea mate mshambuliaji wa Sporting Lisbon Bas Dost. Mchezaji huyu wa umri wa miaka 28 amefunga mabao 36 kwa mechi 41 kwa klabu hiyo ya Ureno. (
Chanzo: ESPN)

Mlinzi wa Manchester United Daley Blind 27, anawindwa na Galatasaray ya Uturuki (
Chanzo: Calciomercato, kupitia Talksport)

Tottenham ilikataa ombi na Nice ya Ufaransa kumnunua mchezaji wa kiungo cha kati Harry Winks, 21, kwa mkopo msimu uliopita. (Chanzo: Daily Mail)

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 31, amethibitisha kuwa nusura ajiunge na Everton msimu uliopita. (
Chanzo: Canal Plus, kupitia Sky Sports)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 10 Octoba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 10 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/10/2017 06:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.