Loading...

Video: Chelsea yatinga robo fainali ya Carabao, ...Westham ikiitoa Tottenham nje ya michuano

Rudiger aliifungia Chelsea bao la kwanza
Kaimu mkufunzi wa Everton David Unsworth amesema kuwa timu yake ilimfurahisha licha ya kutolewa katika mechi ya kuwania kombe la carabao dhidi ya Chelsea.

Willian alifunga bao muhimu la pili huku Chelsea wakisonga mbele na kuingia robo fainali lakini walishangazwa na wageni wao.

Chelsea ilikuwa imeitawala Everton kwa urahisi katika kipindi cha kwanza na kuongoza kupitia kichwa kizuri cha Antonio Rudigers.

Lakini Everton walionekana kuwa hatari baada ya kipindi cha kwanza huku shambulio la Kevin Mirallas likiokolewa naye Ademolar Lookman akipiga mwamba wa goli.

Willian alifunga bao la kimo cha nyoka katika dakika za lala salama kabla ya Dominic calvert kuifungia Everton bao la kufutia machozi.


Katika mchezo mwingine uliochezwa jana, West Ham walisonga mbele katika hatua ya robo fainali baada ya kumudu kujikwamua kutoka mabao mawili nyuma na kumaliza kwa kuifunga Tottenham goli 3-2.

Andre Ayew aliifungia West Ham mabao mawili
Andre Ayew raia wa Ghana ndiye aliyefunga mabao mawili ya mechi hiyo huku Angelo Ogbonna akiongeza la tatu.


Tottenham Spurs ilikuwa imeanza mechi hiyo kwa kishindo pale walipofunga bao la kwanza kwenye dadika 5 tu za mechi hiyo iliyochezwa huko Wembley.

Mpangilio wa timu na mechi za duru inayofuata ya mchuano huo unatangazwa baadae leo.


Video: Chelsea yatinga robo fainali ya Carabao, ...Westham ikiitoa Tottenham nje ya michuano Video: Chelsea yatinga robo fainali ya Carabao, ...Westham ikiitoa Tottenham nje ya michuano Reviewed by Zero Degree on 10/26/2017 03:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.