Loading...

Wanafunzi wachangiswa fedha za walimu

Mbunge wa Same Mashariki, Naghenjwa Kaboyoka
Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, inakabiliwa na uhaba wa walimu hali inayosababisha wanafunzi kuchangishwa Sh10,000 kwa mwezi kwa ajili ya masomo ya ziada.

Miongoni mwa shule zilizoathirika zaidi ni Shule ya Msingi Miamba na Ngujini.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Miamba, Solomon Langeni alisema kuwa tayari wamepeleka malalamiko kwa idara husika lakini hakuna utekelezaji.

“Changamoto hii ni kubwa kwa sisi ambao tupo milimani lakini wenzetu ambao wapo mjini wana walimu wengi,” alisema Mwalimu Langeni. 

Akizungumzia hali hiyo juzi, Mbunge wa Same Mashariki, Naghenjwa Kaboyoka alisema wilaya hiyo ina upungufu mkubwa wa walimu wa shule za msingi na sekondari. Alisema Shule ya Msingi Miamba ina walimu watatu huku ikiwa na zaidi ya wanafunzi 400 na Ngujini ina walimu wawili na zaidi ya wanafunzi zaidi ya 300.

Source: Mwananchi
Wanafunzi wachangiswa fedha za walimu Wanafunzi wachangiswa fedha za walimu Reviewed by Zero Degree on 10/02/2017 08:51:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.