Loading...

Video: Alichokifanya Luis Suarez baada ya kukosa goli Nou Camp kitakushangaza

Suarez akionekana mwenye hasira wakati anaondoka uwanjani
Zilikuwa zimeongezwa dakika 2 tu baada ya dakika 90 za mchezo wa Barcelona dhidi ya Las Palmas kumalizika, ambapo Barca iliibuka na ushindi wa bao 3-0, lakini Suarez alionekana bado hajaridhika na ushindi huo.

Akiichana jezi yake kwa hasira baada ya kukosa goli
Kwa mujibu wa taarifa ya 'Daily Mail', Suarez aliichana jezi yake kwa hasira na kutoka uwanjani baada ya kushindwa kutupia mpira wavuni na kuyafanya matokeo ya mchezo kuwa 4-0 katika dakika ya kwanza ya nyongeza.


Kabla ya tukio hilo, Suarez alikuwa tayari ametoa msaada mkubwa kufanikisha goli moja kati ya magoli mawili aliyofunga Lionel Messi ndani ya uwanja wa Nou Camp uliokuwa hauna mashabiki. Nyota huyo alionekana mwenye hasira wakati anaondoka uwanjani kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kabla ya mchezo kumalizika.


Pamoja na kwamba Uwanja wa Nou Camp haukuwa na mashabiki, Barcelona walifanikiwa kuendeleza ubabe wao ndani ya dakika 90.

Messi aliihakikishia Barca ushindi kwa magoli mawili aliyopachika mnamo dakika ya 70 na 77 na baadae kumsogezea Luis Suarez pasi ya uhakika katika dakika za nyongeza.

Luis Suarez alishindwa kupachika bao baada ya mpira alioupiga kupita pembeni ya goli na kuamua kutoka uwanjani.

Nyota huyo tayari amefunga magoli 2 tu kwa msimu huu baada ya kufanikiwa kupachika magoli 37 katika michezo 51 msimu uliopita.

Video: Alichokifanya Luis Suarez baada ya kukosa goli Nou Camp kitakushangaza Video: Alichokifanya Luis Suarez baada ya kukosa goli Nou Camp kitakushangaza Reviewed by Zero Degree on 10/02/2017 04:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.