Loading...

Hazard kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Uingereza


Kwa mujibu wa taarifa za mitandao, Chelsea wanakaribia kumfanya Eden Hazard kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Taarifa hiyo inadai kwamba, mabingwa hao watetezi, inaonekana watampa mkataba mpya winga huyo utakaomwingizia paundi laki 3 kwa wiki ili kumfanya afute mawazo yake ya kuondoka Chelsea kwenda Real Madrid kuelekea dirisha dogo la usajili mwezi January.

Taarifa zinadai Hazard anaweza kusaini mkataba huo atakaporejea kutoka kwenye majukumu ya kimataifa na timu yake ya Ubelgiji ndani ya wiki chache zijazo kukiwa na ongezeko kubwa kwenye mshahara wake anaolipwa sasa wa paundi laki mbili na ishirini kwa wiki.

Nyota huyo mwenye miaka 26, ambaye hadi hivi sasa ameichezea Ubeligiji michezo 78, hajafanikiwa kupata goli akiwa na Chelsea hadi hivi sasa katika michezo 8 ya michuano yote iliyopita msimu huu, lakini ameshatoa 'assist' 3.


Hazard, ambaye aliwasili Stamford Bridge mwezi Juni mwaka 2012 kufuatia uhamisho wake ulioigharimu Cheslea paundi milioni 32 akitokea Klabu ya Lile ya Ufaransa inayoshiriki Ligue 1, ameshafunga magoli 72 katika michezo 256 aliyoichezea Chelsea kwenye michuano yote na kusaidia klabu yake kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu, moja la Europa na jingine moja la Capital One.
Hazard kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Uingereza Hazard kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Uingereza Reviewed by Zero Degree on 10/02/2017 05:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.