Loading...

Shinyanga: Dawa ya nguvu za kiume yauwa


Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 60 amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu ya kuongeza nguvu za kiume kwa mganga wa kienyeji mkoani Shinyanga.

Kufuatia kifo cha mzee huyo Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mtu mmoja ambaye ni Mganga wa kienyeji ambaye anatuhumiwa kusababisha kifo cha mzee huyo mwenye umri wa miaka 60 wakati anamfanyia matibabu ya kumuongezea nguvu za kiume kwa njia ambayo imetajwa kuwa sio sahihi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga amethibitisha kumshirikia mganga huyo na kudai kuwa upelelezi unaendelea na pindi ushahidi utakapokamilika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Source: EATV
Shinyanga: Dawa ya nguvu za kiume yauwa Shinyanga: Dawa ya nguvu za kiume yauwa Reviewed by Zero Degree on 10/02/2017 05:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.