Loading...

Ajali yaua watu 10 na kujeruhi wengine 24 mkoani Singida.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Debora Magiligimba
Watu kumi wamefariki na wengine ishirini na nne wamelazwa katika hospitali ya Malkia wa ulimwengu Puma na hospitali ya mkoa wa Singida,baada ya magari waliyo kuwa wakisafiria kutoka kwenye sherehe ya harusi na wengine kutoka katika msiba kugongana uso kwa uso.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo pamoja na vifoo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba ambaye alikuwepo eneo la tukio, amesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa mbili usiku tarehe ishirini na tatu wilayani Ikungi, na imesababishwa na uzembe wa dereva wa gari aina ya Toyota Hiace na T.581 BBV kulifuata gari aina ya Toyota Noah namba T.423 CFF na kusababisha vifo na majeruhi.

Majeruhi wakieleza kwa shida huku wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Malkia wa ulimengu Puma wamesema wao waliokuwa wamepanda Hice wakitokea kwenye harusi ghafla wakaona dereva wao aliyetambulika kwa jina moja la Kitundu amehama upande wapili wa barabara na kugongana uso kwa uso na Noha ambayo ilikuwa wapishane nayo.

Kwa upande wake daktari wa hospitali ya Malkia wa ulimwengu daktari John Mmary amesema majeruhi kumina tano waliolazwa katika hopitali hiyo wanaendelea vizuri na matibabu isipokuwa wawili halizao siyo nzuri na wameumia sehemu kubwa za vichwa.

Magari yaliyo gongana aina ya Hice inadaiwa lilikuwa limewabeba maharusi pamoja na ndugu zao huku gari aina ya Noha ilikuwa imewabeba watu walio kuwa wakitokea kwenye msimba.
Ajali yaua watu 10 na kujeruhi wengine 24 mkoani Singida. Ajali yaua watu 10 na kujeruhi wengine 24 mkoani Singida. Reviewed by Zero Degree on 11/24/2017 05:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.