Loading...

Alichosema Mussa Hassan Mgosi kuhusu mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa

Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa
Mshambuliaji nyota wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mussa Hassan Mgosi, amesema kuwa kwenye Ligi Kuu Bara mshambuliaji mbishi uwanjani ni Obrey Chirwa wa Yanga.

Chirwa ambaye amekuwa tishio katika kufunga, mpaka sasa ana mabao sita yakiwa mawili nyuma ya anayeongoza ambaye ni Emmanuel Okwi wa Simba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Global TV Online, Mgosi alisema kwamba, hata kama akichezewa faulo bado mchezaji huyo amekuwa hakati tamaa kiasi cha kuwafanya mabeki wengi kumuogopa.

Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi
“Enzi zangu mimi hata ukinichezea rafu vipi, ndiyo kwanza nakuja kwani straika ukigongwa kidogo halafu ukahama upande unampa kichwa yule beki kuwa kakuweza.

“Katika ligi kuu, kwa sasa straika nunda ni Chirwa kwani ndiye namuona hata ukimchezea rafu vipi bado atakufuata, mwingine ni John Bocco,” alisema Mgosi.

Mgosi alikuwa mmoja wa washambuliaji matata na wasumbufu wanapokuwa uwanjani.

Mshambuliaji huyo aliyetokea Mtibwa Sugar kutua Simba, alikuwa akihofiwa sana na mashabiki wa Yanga kipindi timu hizo zinapokutana.
Alichosema Mussa Hassan Mgosi kuhusu mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa Alichosema Mussa Hassan Mgosi kuhusu mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa Reviewed by Zero Degree on 11/24/2017 04:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.