Loading...

Hakimu amuonya Mama Wema mahakamani

Mama Wema, Miriam Sepetu akitoka mahakamani baada ya kesi hiyo kuahirishwa
Mama Mzazi wa msanii wa filamu za Bongo, Wema Sepetu Miriam Sepetu , ameonywa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba baada ya mtoto wake huyo kutohudhuria mahakamani kwaajili ya kuhudhuria katika kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili.

Wakili wa Serikali Agustino Michael ambaye ni Wakili wa serikali aliitaja kesi hiyo mbele ya hakimu Simba kuwa ndiyo iliyokuwa ikitakiwa kuendelea.

Mama wa mrembo huyo alinyoosha kidole na Hakimu alimkaribisha mama huyo kusema, mama huyo ameiambia mahakama kuwa mwanae ameshindwa kufika mahakamani hapo kwa kuwa amefiwa na shangazi yake hivyo ameenda kushughulikia shughuli za mazishi ndiyo maana hajafika na mimi nimekuja kumuwakilisha.

Baada ya mama huyo kutoa hudhuru huo, Hakimu alimuuliza kama Wema amepatwa na msiba uliomfanya ashindwe kufika mahakamani imekuwaje yeye mama huyo apate muda huo yeye ashindwe?

Hata hivyo Hakimu alimueleza mama huyo na kumuambia asichukulie masihara suala la mstakiwa kuripoti Mahakamani. Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Disemba 14 mwaka huu.
Hakimu amuonya Mama Wema mahakamani Hakimu amuonya Mama Wema mahakamani Reviewed by Zero Degree on 11/24/2017 04:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.