Alonso: Hiki ndicho kikwazo kikubwa kwa Chelsea msimu huu
Beki wa klabu ya Chelsea, Marcos Alonso |
Mhispania huyo anaamini kwamba, ratiba yao ngumu kwenye Kalenda ya Ligi Kuu ya Uingereza katika majira haya ya baridi ndio kikwazo kikubwa kwao katika kutetea taji la ligi hiyo.
Vijana wa Antonio Conte walimaliza Ligi Kuu katika nafasi ya kwanza msimu uliopita, lakini hawakushiriki Ligi ya Mabingwa na hivyo kujikuta wakicheza mechi chache zaidi ya mechi watakazotakiwa kuchezza msimu huu.
Vijana wa Antonio Conte walimaliza Ligi Kuu katika nafasi ya kwanza msimu uliopita, lakini hawakushiriki Ligi ya Mabingwa na hivyo kujikuta wakicheza mechi chache zaidi ya mechi watakazotakiwa kuchezza msimu huu.
Kabla ya yote, meneja wa Chelsea ndiye aliyeanza kulalamikia ratiba ya Ligi Kuu ya Uingereza na sasa Alonso anaonekana kuunga mkono fikra za kocha wake, lakini amesistiza kwamba anajisikia mwenye furaha sana kuelekea mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Qarabag.
Marcos Alonso |
“Tunaelekea katika wakati mgumu sasa, sio kwa wiki hii tu, nadhani kila mtu anajua ni jinsi gani msimu wa Christmas ulivyo Uingereza.” alisema.
“Tutakuwa na mechi kila baada ya siku tatu kuanzia sasa hadi mwanzoni mwa mwezi Februari. Wakati mwingine hatutakuwa sawa kwa asilimia mia moja lakini kila mchezaji anatakiwa kuisaidia timu. Tunatakiwa kujiandaa na kuwa makini.”
“Kuna mechi nyingi hapa katikati. Tunapata majeraha madogo madogo, tunachoka sana, hivyo muda wa kusubiria majeraha yapone ni muhimu.” alisema Alonso na kuongeza:
“Kama itafika hatua nitahisi kushindwa kuisaidia timu, nitamweleza meneja kuwa nimechoka. Lakini najisikia vizuri. Nachukua wasaa wa kupumzika pale ninapoweza na ninashirikiana na timu ya afya kwa asilimia mia moja katika kila mechi.”
Alonso: Hiki ndicho kikwazo kikubwa kwa Chelsea msimu huu
Reviewed by Zero Degree
on
11/22/2017 04:43:00 PM
Rating: