Loading...

Lowassa: "Mabadiliko ya kweli yatatoka nje ya CCM"

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amesema uamuzi wa baadhi ya wanachama wa vyama vya siasa nchini kuhama chama kimoja na kuhamia kingine usichukuliwe kama jambo baya.

Lowassa aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa jambo hilo lisiwe kigezo cha kubaguana na kuwataka wananchi kutanguliza Utanzania.

Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Tanzania alisema yeye binafsi anaamini kuwa mabadiliko ya kweli yanatoka nje ya CCM.

“Hatuwezi kugombana na kuchukiana kwasababu ya Kuhama vyama na wala tusikubali kubaguliwa hivyo, sisi ni Watanzania Kwanza. Lakini binafsi bado naamini Mabadiliko ya kweli yatatoka nje ya CCM.” aliandika Lowassa.
Lowassa: "Mabadiliko ya kweli yatatoka nje ya CCM" Lowassa: "Mabadiliko ya kweli yatatoka nje ya CCM" Reviewed by Zero Degree on 11/22/2017 03:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.