Loading...

Dar: Mfanyabiashara wa risasi mtaani atiwa mbaroni

Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, limesema kuwa tarehe 6, Novemba mwaka huu maeneo ya Serengeti Kigamboni lilipokea taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Willy Peter kuwa anafanya biashara ya kuuza risasi mtaani. Polisi walifanya ufuatiliaji na hatimaye kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na risasi 69 za kivita aina ya FN G3.

Katika mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kuwa risasi hizo alipewa na mtu aliyemtaja kwa jina la Matabu William kwa ajili ya kwenda kuziuza na kwamba alimpatia risasi hizo huko nyumbani kwake Kiwalani jijini Dar es salaam.

Hata hivyo polisi walifika nyumbani kwa Matabu William Matoke (52) kiwalani ambapo alikiri kufanya biashara hiyo ya risasi na alipopekuliwa katika nyumba yake hiyo alikutwa na risasi moja aliyokuwa ameifukia pembezoni mwa nyumba yake na kufanya jumla ya risasi zilizokamatwa kuwa 70.

Aidha Kamanda Mambosasa amesema kuwa watuhumiwa wote wawili wanaendelea kuhojiwa zaidi na upelelezi utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Dar: Mfanyabiashara wa risasi mtaani atiwa mbaroni Dar: Mfanyabiashara wa risasi mtaani atiwa mbaroni Reviewed by Zero Degree on 11/10/2017 05:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.