Loading...

Hospitali ya Muhimbili yafanikiwa kufanya upasuaji wa kupandikiza figo

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikishirikiana na wataalam kutoka Hospitali ya BLK ya New Delhi, India, 2017 wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kihistoria wa upandikizaji wa figo (Renal Transplant).

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi rasmi wa upandikizaji wa figo uliofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

“Kupitia hadhara hii nipende kutumia fursa hii kuwafahamisha rasmi Watanzania kwamba sasa hivi Hospitali yetu ya Taifa ya Muhimbili kwa kushirikiana na Hospitali ya BLK ya New Delhi, nchini India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa upandikizaji wa figo,” alisema Mh. Ummy

Pia Waziri Ummy amesema kuwa kuanzishwa kwa huduma hizi zakibingwa za kupandikiza figo hapa nchini ambazo awali zilikua hazipatikani kutaleta nafuu katika gharama ambazo zingetumika, hii inatokana na ongezeko kubwa la wagonjwa wa figo huku wengi wao wakihitaji huduma ya utakasishaji damu (Renal Dialysis).

Kwa upande mwingine Mh. Ummy ameongeza kuwa Serikali imeanzisha vituo vya utakasishaji damu katika hospitali za Mbeya Rufaa, Chuo Kikuu cha Dodoma, KCMC na Bugando kwaajili ya wagonjwa wanaohitaji huduma za dialysis. Vile vile, huduma hii inapatikana katika hospitali za binafsi hapa Dar es Salaam zikiwemo za Kairuki, TMJ, Regency, Aga Khan, Access na Hindu Mandal.

Mh. Ummy Mwalimu amewahasa Watanzania kuendelea kuiamini Hospitali ya taifa ya Muhimbili kutokana na huduma bora zinazotolewa na amewahakikishia serikali itaendelea kuboresha huduma zaidi katika vituo vyote vya Afya nchini.

Aidha Mh. Ummy Mwalimu (MB) ameendelea kuwakumbusha na kuwahasa Watanzia kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya ili kupunguza gharama kubwa inayoweza kuwakumba pindi watakapopata magonjwa.

Pia Mh. Ummy (MB) hakusita kumpongeza Raisi wa awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa kwa kuwa karibu sana na sekta ya Afya kwa kuboresha huduma za matibabu yakibingwa,

“Wakati Mh. Raisi anaingia madarakani Muhimbili walikuwa wana vitanda vya ICU 21 tu, leo Muhimbili wanavitanda 74, wagonjwa 74 wanaweza kuhudumiwa mara moja kwa wakati mmoja ambao wanahitaji huduma za dharura,” alisema Mh. Ummy Mwalimu.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof. Laurence Museru amewashukuru Madaktari bingwa wa upandikizaji wa figo kutoka Hospitali ya BLK ya New Delhi India kwa kukubali kutoa mafunzo kwa madaktari wa Tanzania bila gharama yoyote.
Hospitali ya Muhimbili yafanikiwa kufanya upasuaji wa kupandikiza figo Hospitali ya Muhimbili yafanikiwa kufanya upasuaji wa kupandikiza figo Reviewed by Zero Degree on 11/25/2017 09:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.