Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 25 Novemba, 2017

Cesc Fabregas na Antonio Conte
Antonio Conte anasema Cesc Fabregas hakustahili kuanza na kikosi cha kwanza cha Chelsea msimu uliopita, lakini anafurahia kiwango kikubwa cha raia huyo wa Uhispania msimu huu.

Emre Can amekubali ofa ya Juventus, na anategemewa kujiunga na mabingwa hao wa Italia mkataba wake na Liverpool utakapomalizika mwisho wa msimu huu.

Nahodha wa klabu ya Liverpool, Jordan Henderson anasema kwamba, maumivu ya kushindwa kupata ushindi kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Sevilla yatawapa motisha ya kuiadhibu Chelsea kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Eddie Howe anasema kwamba, kurejea katika hali nzuri kwa mshambuliaji Callum Wilson ni kama usajili mpya kwa Bournemouth. (Star)

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Argentina na Inter Milan, Mauro Icardi 
Chelsea wana matamanio ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan, Mauro Icardi kwa paundi milioni 100, lakini meneja wa klabu hiyo, Luciano Spalletti anaamini nyota huyo wa Argentina atabakia na Inter hadi mwisho.

Klabu ya Fiorentina imeonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji wa Everton, Henry Onyekuru, ambaye yuko katika klabu ya Anderlecht kwa mkopo, ikitanguliwa na klabu za Manchester United, Barcelona and Juventus. (Sun)

Pep Guardiola anasema hataujali sana mchezo wa Manchester City dhidi ya Huddersfield leo, tofauti Manchester United waliofungwa goli 2-1 msimu huu.

Meneja wa klabu ya Celtic, Brendan Rodgers
Brendan Rodgers anasema kwamba, kichapo cha bao 7-1 ambacho Celtic walichapwa kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya PSG hakijanaribu morali ya wachezaji wake. (Telegraph)

Lionel Messi anamtaka meneja wa Barcelona, Ernesto Valverde amsajili kiungo wa klabu ya Manchester City, Bernardo Silva, licha ya mreno huyo kusajiliwa na klabu hiyo katika majira ya joto.

Manchester United wanatazamia kumsajili nyota wa klabu ya PSG, Javier Pastore, anasistiza shujaa wa klabu hiyo, Eric Cantona.

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameizuia klabu yake kufanya usajili wa nyota wa Inter Milan na Argentina, Mauro Icardi, kutokana na uhusiano wake na mchezaji mwenzake wa Argentina, Lionel Messi.

Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich, Robert Lewandowski
Cristiano Ronaldo amechukizwa na mipango ya klabu ya Real Madrid kutaka kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski.(Express)

Alan Pardew anakaribia kujiunga na klabu ya West Brom kama meneja mpya, ikiwa tayari ameshakutana na uongozi wa klabu hiyo mara mbili wiki hii kufanya mazungumzo juu ya kibarua hicho.

Manchester City wanakaribia kukamilisha dili la kulipwa paundi milioni 50 kwa mwaka na kampuni ya Puma ambalo litawafanya wapunguze tofauti kubwa iliyopo kibiashara kati yao na Manchester United.

Aliyekuwa meneja wa klabu ya West brom, Tony Pulis
Tony Pulis anategemewa kuchukua nafasi ya meneja wa klabu ya Swansea, Paul Clement, endapo klabu hiyo itaamua kumfukuza kazi meneja huyo aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Chelsea na Bayern Munich.(Daily Mail)

Manchester United wanategemewa kumkosa nyota wa Arsenal, Mesut Ozil, ikiwa klabu ya Barcelona tayari imetoa ofa ya kumlipa mshahara wa paundi 350,000 kwa wiki.

Kwa mujibu wa meneja wa Tottenham, Maurcio Pochettino, Davinson Sanchez ni mmoja kati ya viongo bora wa kati duniani na ataboresha kiwango chake hivi karibuni.

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho akizungumza na mshambuliaji wa timu hiyo, Zlatan Ibrahimovic mazoezini
Jose Mourinho amekiri kwamba Manchester United haifungi magoli ya kutosha, lakini hilo halitamlazisha aharakishe kumrejesha mshambuliaji wake, Zlatan Ibrahimovic kikosini. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 25 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 25 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/25/2017 09:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.