Loading...

Huyu ndiye nyota wa Romania anayewindwa na Chelsea


Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Chelsea wanaonekana kuwa na matamanio ya kumsajili nyota wa Romania, Florinel Coman anayechezea klabu ya Steaua BucureÈ™ti.

Katika harakati za kumtafuta mtu sahihi wa kushirikiana na Eden Hazard katika safu ya ushambuliaji, Chelsea sasa wameangukia kwa Coman lakini watatakiwa kulipa kiasi kikubwa cha fedha ili kufanikisha uhamisho huo.

Taarifa iliyotolewa na 'The Sun' inadai kwamba paundi milioni 88 ndizo fedha ambazo zitaweza kuvunja mkataba wa winga huyo lakini kuna uwezekano mkubwa akanunuliwa kwa kiasi cha fedha chini ya hapo kwani aliigharimu București kiasi cha paundi milioni 2 mwezi Agosti.



Sasa kuna taarifa nyingine zinazodai kwamba, mkurugenzi wa benchi la ufundi, Michael Emenalo alienda kumchunguza kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 nchini Romania wiki iliyopita, alipoisaidia Steua kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Dinamo.

Kwa mujibu wa taarifa ya 'Daily Mail', mmiliki wa klabu ya Steau Bucurest, Gigi Becali anamlinganisha kinda huyo na Kylian Mbappe.
Huyu ndiye nyota wa Romania anayewindwa na Chelsea Huyu ndiye nyota wa Romania anayewindwa na Chelsea Reviewed by Zero Degree on 11/02/2017 09:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.