Loading...

Huyu ndiye Rais mpya wa Zimbabwe

Rais Mnangagwa na mkewe Auxillia wakiwasalimia wananchi waliofika kwenye hafla ya kuapishwa kwake
HATIMAYE Zimbabwe imempata rais mpya, Emmerson Mnangagwa, ambaye ameapishwa rasmi kuchukua wadhifa huo kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe aliyeliongoza taifa hilo kwa miaka 37 tangu lijipatie uhuru kutoka wa Waingereza.

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu
Kifuatacho ni kiapo cha Emmerson Mnangagwa alichokitoa leo:

”Mimi Emmmerson Dambudzo Mnangagwa naapa kwamba kama Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe nitakuwa muaminifu kwa Zimbabwe na kuheshimu na kuilinda katiba pamoja na sheria zingine zote za Zimbabwe na nitalinda sheria zote zitakazoendeleza nchi hii na nitapinga chochote kitakachoiathiri Zimbabwe na nitalinda na kuimarisha haki za watu wa Zimbabwe na nitatekeleza majukumu yangu kwa nguvu zangu zote na uwezo wangu wote na nitaheshimu haki za Zimbabvwe na raia wake, ewe mwenyezi Mungu nisaidie”.

Upinzani unamtaka Mnangagwa, ambaye amekuwa mmoja wa watawala, kumaliza “utamaduni wa ufisadi”. Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 Jumanne iliyopita iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe.
Huyu ndiye Rais mpya wa Zimbabwe Huyu ndiye Rais mpya wa Zimbabwe Reviewed by Zero Degree on 11/24/2017 04:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.