Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia), Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Hamdun Mansur (katikati) na Afisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Ndugu Bajuta wakisoma ramani ya Pori Tengefu Loliondo na mpaka wake na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Ngorongoro muda mfupi kabla ya kuanza ziara ya kukagua maeneo hayo
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla amesema viongozi wote ambao waliohusika na rushwa kwenye wizara hiyo watafikishwa kwenye mkono wa sheria.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu Loliondo jana mkoani Arusha.
Kigwangalla ameyasema hayo alipotembelea hifadhi ya Serengeti katika pori tengefu la Loliondo ambapo amesema kuna kikundi ndani ya wizara kimekuwa kikiendesha vitendo vya rushwa kikihusisha wakurugenzi na mawaziri waliomtangulia.
Dk. Kigwangalla (kulia) akimuhoji mmoja ya wananchi jamii ya wafugaji alipotembelea Pori Tengefu Loliondo.
Waziri Kigwangalla (kushoto) akioneshwa mpaka wa Hifadhi ya
Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Pori Tegefu Loliondo na Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Hamdun Mansuri
“Ninafahamu kuwa kuna utaratibu wa ugawaji wa vitalu kinyume na sheria ambao nimeusitisha na nitafuatilia vitalu alivyogawa waziri Nyalandu kinyume na sheria na mkurugenzi aliyekuwepo nitawachukulia hatua”, amesema Kigwangalla.
Kigwangalla amesema kuwa atafukua mafaili yote na kuwaondoa mmoja baada ya mwingine na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wote waliohusika na vitendo hivyo ikiwemo kuwauza wanyama hai nje ya nchi.
Kigwangalla aahidi kumshughulikia Nyalandu na wenzake
Reviewed by Zero Degree
on
11/07/2017 08:25:00 PM
Rating: 5