Kenya: Gavana wa kaunti ya Nyeri afariki katika ajali
Picha ya Ajali hiyo |
Wahome Gakuru enzi za uhai wake |
Alikimbizwa katika Hospitali ya Thika Level 5 kwa matibabu ya dharura lakini akaaga dunia.
Kaunti kamishna wa Murang’a John Elungata alithibitisha kifo hicho.
Bwana Elungata alisema kuwa kabati ni eneo hatari na madereva hukosa mwelekeo kila kunaponyesha.
Inadaiwa kuwa Gavana huyo alikuwa akielekea kuhudhuria kipindi kimoja cha radio na runinga wakati gari lake lilipokumbwa na ajali hiyo.
Daktari Gakuru ni Gavana wa pili wa Nyeri kufariki afisini baada ya Gavana Nderitu Gachagua kufariki mwezi Februari mwaka huu.
Kaunti kamishna wa Murang’a John Elungata alithibitisha kifo hicho.
Bwana Elungata alisema kuwa kabati ni eneo hatari na madereva hukosa mwelekeo kila kunaponyesha.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa gari la gavana huyo lilikuwa na abiria wanne wakati wa ajali hiyo, akiwemo msaidizi wake wa kibinafsi, mlinzi wake na Dereva.
Mkono na mguu wa msaidizi wake wa kibinafsi ilivunjika huku miguu ya mlinzi wake ikijeruhiwa vibaya huku Dereva akidaiwa kuwa katika hali nzuri.
Polisi wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya gurudumo moja la gari hilo kupasuka wakati mvua kali ilipokuwa ikinyesha.

Mwili wa Gavana huyo umesafirishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Lee mjini Nairobi.
Gakuru ni Gavana wa pili wa Nyeri kufariki ndani ya mwaka mmoja |
Daktari Gakuru ni Gavana wa pili wa Nyeri kufariki afisini baada ya Gavana Nderitu Gachagua kufariki mwezi Februari mwaka huu.
Kenya: Gavana wa kaunti ya Nyeri afariki katika ajali
Reviewed by Zero Degree
on
11/07/2017 02:00:00 PM
Rating: