Kikosi cha Chelsea kinachotarajiwa kuivaa Manchester United Jumapili
Meneja wa Chelsea, Antonio Conte |
Akitokea kuuguza majeraha katika paja, kiungo wa klabu ya Chelsea, N'Golo Kante atapewa nafasi ya kuishiriki katika mechi ya Chelsea dhidi ya Manchester United kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.
Danny Drinkwater na N'Golo Kante walipokuwa Leicester City |
Kwa mujibu wa taarifa ya 'Mirror', Kante anaweza kuungana na aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Leicester, Danny Drinkwater, ambaye anategema kuanza na kikosi cha kwanza cha Chelsea kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.
Victor Moses (Chelsea) |
Kikosi cha Chelsea: Courtois, Caballero, Rudiger, Alonso, Fabregas, Drinkwater, Kante, Morata, Hazard, Pedro, Bakayoko, Kenedy, Musonda, Zappacosta, Willian, Batshuayi, Cahill, Christensen, Azpilicueta, Luiz, Clarke-Salter, Scott, Eduardo.
Wakati huo huo, Jose Mourinho, hategemei kuona mchezaji yeyote akirejea kikosini kutoka majeruhi katika mchezo huo utakaochezwa kesho Jumapili.
Manchester United hawakuwa na nyota wao wanne katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Benfica, walipoibuka na ushindi goli 2-0 wakati Jesse Lingard akiumia na kutolewa wakati wa mapumziko siku ya Jumanne.
Paul Pogba, Michael Carrick, Marouane Fellani, Zlatan Ibrahimovic na Marcos Rojo, wote wameshakaa benchi kwa muda wa kutosha kutokana na majeraha.
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho |
Alipoulizwa kuhusu uzito wa mechi inayomkutanisha na timu yake ya zamani, Mourinho alisema: "Sio jambo kubwa. Ni kitu cha kawaida, huu ndio mpira, hapa tunazungumzia utaalamu. Leo utakuwa na klabu hii, kesho utakuwa na klabu nyingine.
"Ni jambo kubwa kwa sababu ni mechi kubwa, sababu ni mpinzani mkubwa, na ni mabingwa. Ni moja ya mchezo mkubwa kati ya timu mbili kubwa ndani ya nchi. Lakini kwa mtazamo wa hisia, ni mechi nyingine zaidi."
Kikosi cha Man United: De Gea, Romero, Pereira, Valencia, Darmian, Tuanzebe, Bailly, Lindelof, Jones, Smalling, Blind, Shaw, Rojo, Young, Matic, Herrera, McTominay, Mata, Mkhitaryan, Lukaku, Rashford, Martial.
Kikosi cha Chelsea kinachotarajiwa kuivaa Manchester United Jumapili
Reviewed by Zero Degree
on
11/04/2017 08:21:00 PM
Rating: