Loading...

Makamu wa Rais nchini Zimbabwe atumbuliwa

Rais Robert Mugabe amemfuta kazi rasmi Makamu wa wake
Makamu wa rais nchini Zimabawe, Emmerson Mnangagwa amefutwa kazi, kwa mujibu wa wizara ya habari nchini humo.

Emmerson Mnangagwa
Mnangagwa, ambaye ana umri wa miaka 75, alionyesha tabia za kukosa uzalendo, alisema waziri Simon Kahaya Moyo.

Kufukuzwa kwake ni ishara kuwa mke wa rais Robert Muabe, Grace, ndiye atakayefuata nyayo za mumeme na kuwa rais wa Zimbabwe

Hivi karibuni, Grace alitoa wito kwa mumewe akitaka amfukuze kazi Emmerson Mnangawa.

Mnangagwa, ambaye alikuwa mkuu wa idara ya ujasusi amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais Mugabe.

Kufutwa kwake kunakuja baada ya Rais Robert Mugabe, 93, kutisha kumfuta Bw Mnangagwa, hatua ambayo imezua uvumi kuwa anataka mke wake amrithi.

Bi Grace Mugabe
Akihutubia wanachama wa makanisa ya asili mji Harare siku ya Jumapili, Bi Mugabe alisema: "Nyoka ni lazima apigwe kwenye kichwa. Lazima tukabiliane na nyoka anayehusika na migawanyiko chamani.Tuneelekea kwenye mkutano tukiwa chama kimoja."

Robert Mugabe alimtaka Mnangagwa na wafuasi wake wachague kuwa wazalendo au awafukuze kazi.

Chama cha Zanu-PF kinatarajiwa kuifanyia mabadiliko katiba yake wakati wa mkutano na kuweka nafasi mbili za makamu wa rais moja ikiwa ni ya mwanamke.

Nafasi hiyo inatarajiwa kujazwa na Bi Mugabe na kuongeza uwezekano wa kumrithi mume wake.
Makamu wa Rais nchini Zimbabwe atumbuliwa Makamu wa Rais nchini Zimbabwe atumbuliwa Reviewed by Zero Degree on 11/06/2017 07:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.