Loading...

Evra afunguka kwa mara ya kwanza baada ya tukio la Alhamis


Patrice Evra amevunja ukimya kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwatumia ujumbe mashabiki wa Marseille baada tukio la kusisimua lilitokea siku ya Alhamis usiku.

Aliyekuwa beki wa kushoto wa Manchester United alitolewa nje kabla ya mechi kuanza baada ya kumpiga shabiki wa timu yake ambayo iliambulia kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Victoria Guimaraes.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali zilizotolewa nchini Ufaransa, mashabiki wa klabu ya Marseille walikuwa wakimtukana beki huyo wakati wa mazoezi ya kupasha mwili kabla ya mechi ya Ligi ya Europa.

Inasemekana kwamba Evra alipiga mpira keulekea walipokuwa mashabiki wa Marseille, kitendo kilichosababisha mambo kuwa mabaya zaidi.

Baada ya muda mfupi baadaye, mfaransa huyo alienda kuwazonga mashabiki hao na kuzuiliwa na wachezaji wenzake.

Kisha Evra alimpiga 
shabiki mmoja wa timu yake, kitendo kilichopelekea atolewe nje ya uwanja kabla ya mechi kuanza na kujikutwa akipewa adhabu ya kukaa benchi na uongozi wa timu yake.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo ya Ligue 1 ilisema: "Rais wa Olympique de Marseille, Jacques-Henri Eyraud, alikutana na Patrice Evra leo na kumpa taarifa juu ya adhabu hiyo na kumuitisha kwenye meza ya mazungumzo kabal ya kuwepo kwa uwezekano wa kuvunja mkataba wake kufuatia vitendo vya ukosefu wa nidhamu."

Mashabiki wa klabu ya Marseille walionyesha hisia zao kufuatia adhabu hiyo aliyopewa Evra kwa kuchapisha mabango yaliyokuwa na sentensi tofauti tofauti wakati wa mechi yao dhidi ya Caen iliyomalizika kwa timu yao kuibuka na ushidni wa goli 5-0.

Bango moja lilisomeka hivi: "Ulifikiri uko juu ya sheria za Taasisi ya Marseille na mashabiki wake," wakati jingine kikisema: "Hatutaki ucheze katika klabu yetu. Ondoka zako."


Mfaransa huyo, ambaye ni mshabiki mkubwa wa mitandao ya kijamii, hakuwa hewani kwenye mtandao wa Instagram tangu tukio hilo limetokea, lakini alirejea na ujumbe kwa mashabiki kufuatia ushindi wa Marseille wa goli 5-0.




Kwa kutumia picha iliyomuonyesha akipiga 'push up' kwenye kioo cha TV, Evra aliandika: "Matokeo ni mazuri sana usiku huu, mmefanya vizuri ndugu zangu, ninajivunia kwa ajili yenu, ..nawashukuru sana mashabiki wa kweli wa Marseille, ...ninapata sapoti kubwa kutoka kwao."

Alijumuisha na ujumbe mwingine uliosema 'Ninaupenda huu mchezo', akirejea maneno yake, na 'kuwa panda', mpango wa ubaguzi wa rangi, ambao yeye pia ni mmoja wa watekelezaji.
Evra afunguka kwa mara ya kwanza baada ya tukio la Alhamis Evra afunguka kwa mara ya kwanza baada ya tukio la Alhamis Reviewed by Zero Degree on 11/06/2017 06:53:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.