Loading...

Polisi yaua majambazi watano mkoani Shinyanga

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule
Majambazi watano waliohusika katika mauaji maeneo ya Kibiti na Mkuranga mkoani Pwani, wameuawa kwa kupigwa risasi na Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Majambazi hao waliokuwa wakituhumiwa kwa mauaji ya Kibiti wameuawa walipokuwa wakitaka kufanya jaribio la kuwapora wafanyabiashara wa dhahabu mjini Shinyanga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amesema mauaji hayo yametokea baada ya jeshi hilo Kitengo cha Intelejensia kupata taarifa ya kuwa kuna majambazi ambao walikuwa wamejipanga kufanya uhalifu.

“Baada ya Polisi kupata taarifa hizo, askari walienda katika eneo hilo ambalo lilikuwa na vichaka pamoja na mapango ambayo yalisababishwa na uchimbaji holela wa mchanga”. Amesema Kamanda Haule

Kamanda Haule amefafanua zaidi kuwa walipofika walianza kurushiana risasi kabla ya kuwazidi na kuwakamata majambazi hao wakiwa wamejeruhiwa vibaya, na wakati wakipelekwa hospitali wote watano walipoteza maisha.

Ameongeza baada ya kuuawa na kupekuliwa, walikutwa na bunduki moja aina ya Short Machine Gun (SMG) yenye risasi 25 pamoja na mabomu mawili ya kurushwa kwa mkono.
Polisi yaua majambazi watano mkoani Shinyanga Polisi yaua majambazi watano mkoani Shinyanga Reviewed by Zero Degree on 11/06/2017 03:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.