Loading...

Makonda atoa zawadi ya gari kwa kamanda wa kikosi cha usalama barabarani jijini Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameagiza kukamatwa kwa madereva wote wanaovunja Sheria za Usalama Barabarani kwakuwa wamekuwa chanzo cha ajali.

RC Makonda amesema hayo kwenye Uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambapo amewataka Askari wa Usalama kusimamie Sheria kikamilifu lakini wahakikishe hakuna uonevu.

Katika uzinduzi huo Makonda amemzawadia gari ya kisasa aina ya Mingle5 Pickup aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Dar es Salaam Kamanda Awadhi Haji kama motisha kutokana na kazi kubwa na nzuri aliyoifanya katika kupunguza msongamano wa magari, ajali na kuwaadhibu madereva wanaotanua Barabarani kwenye mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema ataendelea na utaratibu wa kuwapongeza watumishi wanaofanya vizuri ili kujenga motisha ya watu kufanya kazi kwa bidii.

Aidha RC Makonda amewataka madereva wa vyombo vya moto kuheshimu alama za barabarani ikiwemo zebra na taa za barabarani.

Amesema lengo la serikali ni kuona hakuna mwananchi anaepoteza maisha kwa ajali za uzembe huku akiwapongeza madereva wa bodaboda na bajaji kwa kuanza kubadilika na kuzingatia sheria.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwemo Mkuu wa Usalama barabarani Tanzania Kamanda Fortunatus Muslim, Kamanda Kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Usalama Barabarani Dar es Salaam, Kamanda wa Polis Kinondoni pamoja na kamati za Usalama Barabarani ambapo wamesema wamejipanga kuhakikisha kuwadhibiti madereva wasiozingatia sheria.
Makonda atoa zawadi ya gari kwa kamanda wa kikosi cha usalama barabarani jijini Dar Makonda atoa zawadi ya gari kwa kamanda wa kikosi cha usalama barabarani jijini Dar Reviewed by Zero Degree on 11/19/2017 03:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.