Loading...

Makamu wa Rais, Mama Samia alivyomtembelea Lissu hospitali


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, alienda hospitali kumuona mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu, ambaye amelazwa kutokana na kupigwa risasi.

Mama Samia ambaye alikuwa jijini Nairobi kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, aliwasili hospitalini hapo jioni ya jana akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chana.

Makamu wa Rais mama Samia Suluhu anakuwa kiongozi wa kwanza mkubwa kitaifa kwenda kumuona mbunge huyo ambaye yupo hospitalini hapo tangu Septemba 7 alipopigwa risasi na watu ambao hawajajulikana mpaka sasa.
Makamu wa Rais, Mama Samia alivyomtembelea Lissu hospitali Makamu wa Rais, Mama Samia alivyomtembelea Lissu hospitali Reviewed by Zero Degree on 11/29/2017 09:29:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.