Loading...

Mechi zote ambazo Salum Mayanga ameingoza Taifa Stars


Leo November 12, 2017 kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinacheza mchezo wa kirafiki ya kalenda ya FIFA ugenini dhidi ya Benin, ni mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa Stars chini ya uongozi wa Salum Mayanga kucheza nje ya Tanzania. Kabla ya hapo mechi zote za kirafiki zilikuwa zikichezwa uwanja wa nyumbani.

Stars inaingia kwenye mchezo huo chini ya Mayanga ikiwa imecheza mechi 13, imeshinda michezo 6, sare 6 huku ikiwa imepoteza mchezo mmoja tu. Katika mechi hizo Stars imefunga jumla ya magoli 15 na kuruhusu kufunga magoli 9 na kufanya wastani wa magoli kuwa 6.

Mechi 13 ambazo kocha Salum Mayanga ameiongoza Stars tangu alipokabidhiwa jukumu hilo kutoka kwa Charles Boniface Mkwasa mwezi Machi mwaka 2017:

  • Tanzania 2-0 Botswana (mechi ya kirafiki ya kimataifa)
  • Tanzania 2-1 Burundi (mechi ya kirafiki ya kimataifa)
  • Tanzania 1-1 Lesotho (kufuzu AFCON)
  • Tanzania 2-0 Malawi (COSAFA)
  • Angola 0-0 Tanzania (COSAFA)
  • Tanzania 1-1 Mauritius (COSAFA)
  • Afrika Kusini 0-1 Tanzania (COSAFA)
  • Zambia 4-2 Tanzania (COSAFA)
  • Tanzania 0-0 Lesotho (Stars ilishinda kwa penati 4-2 COSAFA)
  • Tanzania 1-1 Rwanda (kufuzu CHAN)
  • Rwanda 0-0 Tanzania (kufuzu CHAN)
  • Tanzania 2-0 Botswana (mechi ya kirafiki ya kimataifa)
  • Tanzania 1-1 Malawi
Mechi zote ambazo Salum Mayanga ameingoza Taifa Stars Mechi zote ambazo Salum Mayanga ameingoza Taifa Stars Reviewed by Zero Degree on 11/12/2017 04:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.