Loading...

Nyalandu: Sikufukuzwa CCM bali nilijiuzulu kwa mapenzi yangu mwenyewe


Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amekanusha taarifa za kwamba alifukuzwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema aliamua mwenyewe kujiuzulu na kusema kwamba alifanya hivyo wa mapenzi yake pasipo kushinikizwa na mtu.

Mh. Nyalandu amesema hayo alipofanya mahojiano maalumu na chombo cha habari nchini na kusema kwamba taarifa ambazo zinadai kwamba amejiuzulu Ubunge baada ya kufukuzwa CCM si za kweli na kudai ili mtu afukuzwe Uanachama lazima kuna utaratibu ndani ya chama ufuatwe ikiwa pamoja na kuitwa kwenye kamati ya maadili ya chama na kusema kwamba mpaka anatangaza habari za kuachia ngazi hajawahi kuitwa kwenye kamati yoyote wala kupokea barua ya kufukuzwa hivyo habari hizo hazina ukweli.

"Siyo kweli kwamba nilifukuzwa kwenye chama. Nilijiuzulu kwa mapenzi yangu mwenyewe. Sikupata barua yoyote ya kunifukuza hivyo dhana inayodai kwamba nilifukuzwa haina ukweli. Kwa utaratibu wa Chama huwa hufukuzwi kwa barua bali kuna vikao lazima vikae na mimi sikuitwa katika kikao chochote. Pia ikumbukwe mimi sikuwa mwanachama wa kawaida, nilikuwa Mbunge lakini pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM" alisema Nyalandu. 

Hata hivyo Nyalandu amefafanua kuhusu kurudia kugombea kwenye jimbo lake kwa tiketi ya CHADEMA "Mapema sana kuweka wazi kwamba nitagombea au La kwa sababu vyama vina utaratibu wa kumpata mgombea hivyo ndani ya chama tutaangalia atakayeweza kupatiwa nafasi"

Pamoja na hayo Mh. Nyalandu ameongeza kwamba

“Tujikite katika kuwafanya watanzania wanakuwa wamoja hata kama wana tofauti za kiitikadi na mitazamo ya kisiasa kama vile dini na makabila tusiruhusu mmonyoko unaotokana na tofauti zetu tuchukue kwamba tofauti tulizonazo zinatujenga zinatuimarisha kama taifa na zinatufanya tuwe watu wamoja na tusiogope ushindani kwani uleta mema popote unapofanyika katika ustaarabu na kwa uzuri,” Nyalandu

Mh. Nyalandu Oktoba 30 alitangaza kujivua Ubunge wa Singida Kaskazini na nafasi zote za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kutangaza nia ya kujinga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Huku Bunge likitoa taarifa kwamba halijapokea barua ya kujizulu kwake ubunge na kwamba wamepokea taarifa za kuvuliwa uanachama wake na CCM.
Nyalandu: Sikufukuzwa CCM bali nilijiuzulu kwa mapenzi yangu mwenyewe Nyalandu: Sikufukuzwa CCM bali nilijiuzulu kwa mapenzi yangu mwenyewe Reviewed by Zero Degree on 11/03/2017 06:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.