Loading...

Ronaldo amtaja mchezaji atakayeiokoa Real Madrid msimu huu


Cristiano Ronaldo anaamini kurejea kwa Gareth Bale kutaweza kuisadia Real Madrid indokane na hali mbaya ya sasa.

Real Madrid wako nyuma ya vinara wa La Liga, FC Barcelona kwa pointi nane na wamepoteza mechi mbili mfululizo ndani ya wiki moja.
 

Wikendi iliyopita Madrid walichapwa goli 2-0 na Girona, ambao ni wageni katika La Liga kufuatia kupanda daraja msimu huu na Jumanne iliyopita pia walikubali kichapo cha goli 3-1 kutoka kwa Tottenham kwenye Ligi ya Mabingwa.

Cristiano Ronaldo anaamini kurejea kwa Bale kutaipa nguvu Barcelona
Kwa upande wake mshambuliji wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo, yeye anaamini kikosi chao kitaondokana na mkosi huo kwa Bale na Dani Carvajal kurejea kikosini watakapoikaribisha Las Palmas Bernabeu siku ya Jumamosi.


Kwa mujibu wa taarifa ya 'Mirror', nyota huyo wa Ureno alisema: "Wachezaji waliowasili katika majira ya joto wanauwezo mkubwa.


"Pepe, Alvaro Morata na James Rodriguez walitufanya tuwe na nguvu zaidi, lakini walio wengi katika kikosi chetu cha sasa bado ni wachanga.


"Tunahitaji Carvajal na Bale warejee katika hali zao.

"Kikosi siyo kibaya sana lakini hakina uzoefu na ndicho kitu kikubwa. Hakuna jinsi, muda utasema."
Ronaldo amtaja mchezaji atakayeiokoa Real Madrid msimu huu Ronaldo amtaja mchezaji atakayeiokoa Real Madrid msimu huu Reviewed by Zero Degree on 11/03/2017 07:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.