Loading...

Ronaldo amwambia wakala wake anataka kujiunga na klabu ya EPL


Kwa mujibu wa taarifa ya 'Don Balon', Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amemwambia wakala wake, Jorge Mendes afanye mipango ya kurejea Ligi Kuu ya Uingereza.

Ronaldo akiwa na Wakala wake, Jorge Mendes
Hata hivyo, sio klabu yake ya zamani, Manchester United ambayo nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 anataka kujiunga nayo. Inasemekana Mreno huyo anatamani kujiunga na Chelsea mwishoni mwa msimu huu.

Ronaldo hana furaha msimu huu akiwa na Real Madrid kama ilivyozoeleka na amefunga goli 1 tu katika mechi 7 za La Liga hadi hivi sasa. Pia alithibitisha kutosaini mkataba mpya Bernabeu.


Pamoja na kesi inayomwandama ya kukwepa kulipa kodi ya karibuni Euro milioni 15, kumekuwepo na uvumi kwamba anataka kuondoka Uhispania na kurejea nchini Uingereza. Pia imeripotiwa kuwa kuna ugomvi kati yake na nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos, ambapo wawili hao wamekuwa wakitupiana maneno kwenye vyombo vya habari hivi karibuni.

Licha ya kuitumikia klabu ya Manchester United kwa misimu sita, ambapo alishinda Taji la Ligi ya Mabingwa mwaka 2008, inaonekana kwamba Ronaldo anapendelea kuhamia Stamford Bridge.

Manchester United wanatazamia kusajili wachezaji wenye umri mdogo kwa sasa, na nyota huyo wa Real Madrid anaelekea kutimiza miaka 33 mwezi Februari, hivyo ni dhahiri kabisa hawezi kuwa kwenye mipango yao.

Hata hivyo, Cristiano Ronaldo bado hajataka kuhamia Ligi Kuu ya Marekani au kurejea Ureno na anahisi kwamba amebakiwa na miaka kadhaa ya kuendelea kushindania nafasi ya juu.

Neymar Jr
Kwa upande mwingine, klabu ya Real Madrid imekuwa ikihusishwa na Neymar wiki kadhaa zilizopita, ambaye anaweza kuchukua nafasi ya Ronaldo endapo ataamua kurejea Ligi Kuu ya Uingereza katika majira ya joto mwakani.
Ronaldo amwambia wakala wake anataka kujiunga na klabu ya EPL Ronaldo amwambia wakala wake anataka kujiunga na klabu ya EPL Reviewed by Zero Degree on 11/18/2017 01:01:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.