Serikali kuajiri walimu 1600 wa sayansi mwezi Disemba 2017
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI (Elimu), TIXON NZUNDA |
Akizungmza na walimu wa shule ya sekondari Bogwe wilayani Kasulu mkoani Kigoma, NZUNDA amesema kwa sasa serikali imeweka kipaumbele kuajiri walimu wa masomo ya sayansi ambao ndio mahitaji makubwa kwa shule za sekondari ikilinganishwa na walimu wa masomo mengine na kwamba walimu hao watagawanywa katika shule zote za sekondari nchini ili kupunguza tatizo la walimu wa sayansi.
Aidha NZUNDA amesema kuanzia sasa hakutakuwa na uataribu wa kuwapandisha daraja walimu kila baada ya miaka mitatu na badala yake mwalimu atapanda daraja kutokana na jitihada zake katika kufundisha ambapo pia amebainisha kuwa serikali imedhamiria kumaliza madeni mbalimbali ya madai ya walimu ifikapo mwezi wa sita mwakani.
Source: ITV
Serikali kuajiri walimu 1600 wa sayansi mwezi Disemba 2017
Reviewed by Zero Degree
on
11/20/2017 11:52:00 AM
Rating: