Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 20 Novemba, 2017

Paul Pogba na Lukaku wakishangilia bao
Paul Pogba amemtaja mchezaji mwenzake, Romelu Lukaku kuwa ndiye straika bora zaidi kwenye Ligi kuu ya Uingereza.

Daniel Sturridge yuko tayari kuondoka Liverpool mwezi Januari kuokoa ndoto zake za kushiriki kombe la dunia.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola anaweza kuingia kwenye vita ya kusaka saini ya Virgil van Dijk baada ya kuthibitisha kwamba atatafuta beki mpya mwezi Januari.

Danny Rose yuko tayari kurejea kwenye kikosi cha Tottenham kitakachoivaa  Borussia Dortmund Jumanne usiku.

Golikipa wa Tottenham, Hugo Lloris
Hugo Lloris amewaonya wachezaji wenzake wa Tottenham kusahau kuhusu mbio za ubingwa na kuwazia kumaliza katika nne bora msimu huu.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa Manchester City hawazuiliki katika mbio za ubingwa msimu huu kwa sababu wachezaji wao wanatoka nje ya dunia hii. (Mirror)

Pep Guardiola hatamruhusu mchezaji yeyote wa Manchester City kufanya mzaha uwanjani.

David Brooks
Kiungo wa Sheffield United, David Brooks anawindwa na klabu ya Liverpool and Tottenham.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo alizungumza na Antoine Griezmann kuhusu mipango yake ya kuihama klabu hiyo baada ya mechi yao na Atletico Madrid.

Ripoti zinadai kuwa klabu ya Barcelona imetoa ofa kwa ajili ya kumnasa nyota wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil. (Express)

Benevento wamekuwa na mwanzo mbaya zaidi kuliko timu yoyote ile kutoka Ligi 5 bora za Ulaya katika msimu huu kwa kupoteza michezo 13 mfululizo baada ya kuchapwa na Sassuolo Jumapili. (Daily Mail)

Jose Mourinho atakuwa meneja wa Manchester United angalau hadi kufikia mwaka 2020.

Chris Coleman
Meneja wa Sunderland, Chris Coleman amepewa ahadi ya paundi milioni 1 kama atafanikiwa kuirejesha klabu hiyo kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. (Star)

Danny Rose alikerwa na kitendo cha kuachwa kwenye kikosi kilichoivaa Arsenal Jumamosi.

Sam Johnstone anawindwa na klabu ya West Brom na anaweza kumaliza haraka mkataba wake wa mkopo Aston Villa. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 20 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 20 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/20/2017 11:26:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.