Loading...

Ronaldo amkasirikia kocha na wachezaji wenzake baada ya sare dhidi ya Atletico


Mambo yalizidi kuwa mabaya zaidi kwa Cristiano Ronaldo kufuatia sare ya bila kufungana katika mechi dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid Jumamosi alipohamishia hasira zake kwa kocha Zinedine Zidane na baadhi ya wachezaji wenzake.

Ronaldo anapitia kipindi kigumu kwake katika suala zima la kuifungia timu yake, akiwa amefunga goli moja tu hadi hivi sasa katika mechi nane za La Liga msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mirror, nahodha huyo wa Ureno ni miongoni mwa wachezaji sita wa La Liga ambao hawajaonekana wakikaba na kuzuia pasi yoyote msimu huu. Wanne wakiwa ni magoli kipa na watano bado hajacheza hata mchezo mmoja.

Taarifa ya tovuti ya 
Diario Gol nao inadai kwamba mambo yalikuwa mabaya zaidi kiasi cha nyota huyo kumweleza kila kitu kwa hasira meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane baada ya mechi kumalizika.

Taarifa inadai kamba, Ronaldo alisema kuwa anajitoa kwa kila kitu uwanjani lakini anakuwa mtu wa kwanza kulaumiwa kwa Real Madrid kuwa na matokeo mabaya.

Mapema mwezi huu, nahodha huyo wa Ureno aliilaumu klabu yake hadharani kwa kuwauza wachezaji wengi muhimu kama Pepe, Alvaro Morata and James Rodriguez.

Lakini safari hii, haikuwa Zinedine Zidane pekee aliyekumbwa na gadhabu ya Ronaldo. Isco, Luka Modric na Marco Asensio pia walihusika, ambapo mshambuliaji huyo aliwatupia lawama wachezaji wenzake kwa kushindwa 'kumtafuta' awapo uwanjani.

Ronaldo anaamini hakuweza kuonyesha kiwango kizuri kwa vile hakupata msaada wowote kutoka kwa wachezaji wenzake.
Ronaldo amkasirikia kocha na wachezaji wenzake baada ya sare dhidi ya Atletico Ronaldo amkasirikia kocha na wachezaji wenzake baada ya sare dhidi ya Atletico Reviewed by Zero Degree on 11/20/2017 01:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.