Loading...

Utafiti: Kulalia mgongo ni hatari kwa mwanamke mjamzito


Wanawake wameshauriwa kulala kwa kutumia upande katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito kuzuia kujifungua watoto waliofariki tumboni.

Utafiti wa zaidi ya wanawake 1000 ulibaini kuwa hatari ya mtoto kufariki tumboni miongoni mwa wanawake wajawazito inaongezeka marudufu iwapo watalalia migongo yao katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito.

Utafiti huo ulichunguza mimba 291 zilizoharibika na wanawake 751 waliofanikiwa kupata watoto.

Watafiti wanasema kuwa upande ambao wajawazito hulalia ni muhimu sana na kwamba hawatakiwi kuwa na hofu yoyote wanapoamka na kugundua wamelalia migongo yao.

Takriban mimba 225 nchini Uingereza huishia kuharibika na watafiti hao wanakadiria kwamba takriban maisha ya watoto 130 kila mwaka yataokolewa iwapo wanawake wataendelea kulalia upande wa kulia ama kushoto.

Utafiti huo wa MiNESS uliochapishwa katika jarida la Kujifungua ni mkubwa wa aina yake na unathibitisha tafiti ndogo za nchini New Zealnd na Australia.
Utafiti: Kulalia mgongo ni hatari kwa mwanamke mjamzito Utafiti: Kulalia mgongo ni hatari kwa mwanamke mjamzito Reviewed by Zero Degree on 11/20/2017 05:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.